maadili kwanza
Sisi ni nani ?Kuhusu Sisi

Maadili Kwanza

Maadili Kwanza Tanzania ni taasisi inayojikita katika kushughulikia changamoto za mmomonyoko wa maadili zinazokabili jamii ya leo, hususan kwa vijana. Tunafanya hivyo kupitia tafiti, elimu ya maadili, mijadala ya wazi na programu za vitendo zinazolenga kubadili namna watu wanavyofikiri, kuamua na kuishi.

Tunaamini kuwa maadili si nadharia pekee, bali ni nyenzo ya maisha inayogusa elimu, kazi, mahusiano, afya, uchumi na uongozi. Kupitia mbinu shirikishi, tunawawezesha watu binafsi na makundi mbalimbali kuelewa wajibu wao katika kujenga jamii yenye maadili na mustakabali bora wa taifa.

Uendeshaji wa taasisi unazingatia katiba yake, misingi ya uwazi na ushiriki wa wanachama, huku marekebisho yakifanyika kwa pamoja kadri mahitaji ya jamii yanavyobadilika.

  • Taasisi hii haifungani na upande wowote wa siasa wala dini
Soma Zaidi
Shiriki sasa Programu

Promramu Zetu