AFYA IMARA

AFYA IMARA

  • $4800 Raised Of $19000

Programu ya Afya Imara inalenga kuimarisha uelewa wa uhusiano kati ya maamuzi ya kimaadili na afya ya mwili, akili na jamii. Inashughulikia masuala kama uraibu wa dawa za kulevya, afya ya akili, lishe, mazoezi na maamuzi yenye athari za muda mrefu kama vile utoaji mimba. Kupitia elimu, ushauri nasaha na majukwaa ya kijamii, programu inalenga kujenga nidhamu binafsi, uwajibikaji wa maisha na kusaidia watu kubadilika kwa hiari na kuwa rasilimali chanya kwa jamii.

Makundi yanayolengwa:

  • Vijana na watoto
  • Walimu na wasimamizi wa watoto
  • Wafungwa na manusura wa kujiua
  • Walezi na waathirika wa magonjwa ya afya ya akili
  • Walezi na waathirika wa ukimwi na VVU
  • Waraibu na watumiaji wapya wa dawa za kulevya
  • Walezi na waathirika wa magonjwa ya yasiyoambukizwa
  • Viongozi wa dini, siasa na mila

Lengo:

  • Kujenga hali ya nidhamu binafsi kwa kuzingatia mlo kamili, mazoezi na mapumziko
  • Kujenga hali ya uwajibikaji wa maisha ya mtu binafsi na wengine kwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa halali
  • Kutoa mafunzo ya kufanya maamuzi yenye athari chanyaa na manufaa ya muda mrefu kwa mtu binafsi na jamii kw aujumla
  • Kuwasaidia waraibu wa matumizi ya dawa za kulevya kuacha kwa hiari na kuwa mfano bora kwa wengine
  • Kujenga raia wema wenye hali ya uzalendo na kujituma kujenga taifa lao bila kuathiri kanuni za maadili na sheria za nchi