JAMII IMARA
Programu ya Jamii Imara inalenga kuifanya jamii kuwa mshiriki mkuu katika malezi na usimamizi wa maadili. Inashirikisha viongozi wa dini, elimu, michezo, siasa, uongozi wa jadi/mila na wadau wengine wa kijamii katika kujenga uwajibikaji wa pamoja. Programu inalenga kuunda mazingira ambayo maadili yanatekelezwa kwa vitendo katika maisha ya kila siku, kwa kuimarisha mifumo ya uangalizi wa watoto na vijana, pamoja na kukuza maadili ya uwajibikaji, mshikamano na uadilifu katika ngazi zote za jamii.
Makundi yanayolengwa:
- Waangalizi wa watoto na vijana nje ya familia
- Taasisi za dini, elimu, michezo, siasa, Uchumi na utawala
- Viongozi wa kijamii na wa jadi (Machifu na viongozi wa kimila)
- Raia wote katika maeneo ya kazi, michezo/burudani, usafiri na huduma za kijamii
Lengo:
- Kushirikisha Jamii katika malezi ya pamoja
- Kutengeneza uwanja wa maadili kwa vitendo na uhalisia
- Kujenga jamii yenye kuwajibika juu ya muenendo wa watu wake kimaadili
- Kujenga jamii imara chini ya misingi ya Umoja, Amani,na Uzalendo kwa maslahi mapana ya Taifa
- Kujenga jamii shindani katika maendeleo bila kuathiri wala kuathiriwa na mitazamo ya kisiasa, kidini na kabila