Programu ya Kazi Imara inalenga kukuza uadilifu, nidhamu na uwajibikaji katika mazingira ya kazi, hususan kwa sekta zisizo rasmi kama wafanyakazi wa ndani, watunza bustani, wafanya usafi, walinzi, madereva wa umma na binafsi, wapishi na wahudumu. Programu inajikita katika kuwajengea wafanyakazi na waajiri uelewa wa mipaka ya madaraka na itifaki, heshima kazini, na umuhimu wa kufanya maamuzi ya kimaadili. Lengo ni kupunguza vitendo vya unyanyasaji, rushwa, hujuma na uzembe kazini, huku ikiongeza bidii, weledi na utu katika utendaji wa kazi kwa manufaa ya mtu binafsi, kampuni na jamii kwa ujumla.
Makundi yanayolengwa:
Lengo: