UCHUMI IMARA

UCHUMI IMARA

Programu ya Uchumi Imara inalenga kuchunguza na kuimarisha uhusiano kati ya maadili na maendeleo ya kiuchumi. Inalenga kuwajengea vijana, wafanyakazi, wafanyabiashara na wajasiriamali uelewa wa namna mmomonyoko wa maadili unavyoathiri uchumi binafsi na wa taifa. Kupitia tafiti, mafunzo na mijadala ya kitaaluma, programu inakuza nidhamu ya kifedha, uaminifu katika biashara, uwekezaji wenye maadili na matumizi sahihi ya rasilimali na fursa zilizopo.

Makundi yanayolengwa:

  • Wajasiliamali na wafanyabiashara
  • Vijana wasio na kazi
  • Waajiliwa na waliojiajili
  • Wawekezaji

Lengo:

  • Kutoa elimu Jinsi mmomonyoko wa maadili unavyodhoofisha uchumi wa mtu, jamii ya Taifa kwa ujumla
  • Kutoa elimu ya maadili na nidhamu ya utunzaji, uwekezaji na ujasiriamali
  • Kutoa elimu jinsi kutumia fursa zilizopo kuingiza kipato bila kuathiri maadili
  • Kujenga hali ya kujituma, ubunifu na bidii ya kazi ili kwenda na kasi ya ushindani wa dunia