WAZAZI/WALEZI IMARA

WAZAZI/WALEZI IMARA

  • $4800 Raised Of $19000

Programu hii inalenga kuimarisha maadili katika mifumo ya malezi kwa wazazi na walezi wa mazingira tofauti. Inalenga kuboresha mahusiano ya wazazi, wachumba na wanandoa kama msingi wa malezi yenye uwajibikaji na tija. Kupitia mafunzo, majukwaa ya majadiliano na ushauri wa kimaadili, programu inalenga kuongeza uelewa wa wajibu wa wazazi na walezi katika kulea watoto wenye maadili thabiti, utambuzi wa kusudi la maisha, lengo la kuishi na uwezo wa kuchangia maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla kwa kuishi maisha yenye kuacha alama chanya.

Makundi yanayolengwa:

  • Malezi ya mzazi mmoja
  • Malezi ya watoto wa ndugu / watoto wa nje
  • Malezi ya yatima
  • Wachumba na wanandoa (wenye watoto na wasio na watoto)

Lengo:

  • Kuimarisha mbinu za malezi yenye kujenga na kuimarisha maadili kwa mtoto
  • Kuboresha mahusiano ya wazazi kama kielelezo cha maadili
  • Kubadili mitazamo kwa kupandikiza hali ya utambuzi juu ya maisha na kwanini wanapswa kuwa wazazi au walezi wenye kuwajibika ili kuhakikisha malezi yenye kusudi na matunda
  • Kutoa elimu ya malezi yenye kuendana na kasi ya sayansi na teknolojia bila kuathir maadili